Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steve Nyerere: Amjibu Mwana FA, ampa saa 48 aombe radhi "Sing'oki Kamwe"

Video Archive
Tue, 22 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MUIGIZAJI Steve Nyerere, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa msemaji wa shirikisho la muziki nchini, leo Machi 22, 2022, amezungumza na wanahabari kuhusiana na yanayoendelea baada ya wasanii wengine kuibuka na kumpinga.

"Nampa masaa 48 awaombe radhi wale wote aliowafedhehesha... Amuombe radhi kiongozi aliyemuita Zumaridi, awaombe radhi wanamuziki wa taarabu, dansi, kwaya na uongozi wa Shirikisho la Muziki [Tanzania].

"Atakayeleta chokochoko za kutaka kutugawanyisha [Tasnia ya muziki], viherehere tupo, tutamgawana yeye. Mimi siwezi kung'ooka kihuni kuhuni tu eti umekuja, 'natoa saa 48,' poor. Sisi tunahitaji saa 48 za kufanya kazi... Hatuwezi [tasnia ya muziki] kugawanyishwa na mtu, labda nisiwepo duniani.

"Kikao kilichofanyika jana kimevunja katiba. Shirikisho wanachama wake ni vyama, sio individual musician [mwanamuziki mmoja mmoja]. Wanavyoongea hapa wanamuziki wanajifurhisha tu, walitakiwa kupeleka malalamiko kwenye vyama vyao.

"Atakayeleta chokochoko za kutaka kutugawanyisha [Tasnia ya muziki], viherehere tupo, tutamgawana yeye.

"Nitajiuzulu kama mwenyekiti, makamu mwenyekiti, bodi ya shirikisho watakaa kama walivyoni-approach [fuata] kuniletea barua, tukakaa vikao. Nitatoka hadharani kusema, hili ndugu zangu naachia ngazi," amesema Msemaji wa SMT, Steve Nyerere.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live