Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa Nigeria amtetea Diamond kukopi nyimbo 'mwacheni apumue'

Diamond Platinumz Spyro Spyro na Diamond.

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa siku chache zilizopita blog za Nigeria kutoa taarifa na kuweka orodha ya ngoma ambazo supastaa wa Bongo Fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz alidaiwa kuwa amekopi, sasa msanii kutoka huko huko Nigeria, Oludipe Oluwasanmi David maarufu kama Spyro ameibuka na kupinga tuhuma hizo kwa Diamond.

Spyro amewataka watu kuacha kumshambulia #Diamond. Kuupitia ukurasa wake wa Twitter, msanii huyo amedai kuwa kila mtu huwa anatoa mawazo kutoka sehemu mbalimbali.

"Hakuna mtu ni kisiwa cha pekee yake, sote tunapata mawazo yetu kutoka maeneo mbalimbali, ukubali au ukatae, Diamond ni mtu wangu, tumeachia wimbo pamoja na amefanya vizuri humo, mwacheni Diamond apumue," amesema Spyro.

Mitanfdao ya kijamii na blogs hizo za Nigeria zilieleza kuwa wimbo wa #Enjoy (Diamond ft Jux) idea yake ni kutoka kwenye ngoma yake "Who's your guy".

#Spyro na #Diamond wameachia wimbo wao mpya uitwao "For you" wakiwa pamoja na #Teni na #Iyanya.

Kwa sasa #Diamond ameshaondoka nchini Tanzania na yupo kwenye ziara yake nchini Canada.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: