Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Snoop Dogg akumbuka Malkia alivyomuokoa asitimuliwe

Snoop D Elizabeth Snoop Dogg akumbuka Malkia alivyomuokoa asitimuliwe

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka Marekani Snoop Dogg amekumbuka mchango wa Hayati Malkia Elizabeth kutokana na mambo aliyowahi kumfanyia enzi za uhai wake.

Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘Capital FM’ juzi Snoop aliweka wazi kuwa Malkia alikuwa shabiki yake sana na ndio maana alifanikisha msanii huyo asifukuzwe nchini Uingereza.

Mwaka 1993 Snoop, alishitakiwa kwa mauaji na kufutiwa mashitaka hayo mwaka 1996 baada ya kutokuwa na hatia huku Malkia akizuia ‘rapa’ huyo asifukuzwa Uingereza wakati alipokwenda nchini humo kwa ajili ya ziara yake.

Kufuatia mahojiano yake ya hivi karibuni, aliweka wazi kuwa Malkia alimtetea asifukuzwe kutokana na wajukuu zake kukubali ngoma zake.

“Walipojaribu kunifukuza kutoka Uingereza, Malkia alitoa maoni kwamba wajukuu zake walimpenda Snoop Doggy na hakufanya kosa nchini Uingereza, kwa hivyo alinipa ruhusa ya kuwa nchini hapo muda wote.”

Malikia Elizabeth II alifariki mwaka 2022, akiwa na umri wa miaka 96, kwa mujibu wa BBC Malikia alifariki kwa Amani nyumbani kwake Balmoral.

Snopp aliwahi kutamba na ngoma nyingi baadhi ni kama Drop it like it's Hot, Next Epsode, Sweat na Let it Roll.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live