Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sijui kama nitaeleweka katika hili

Nitaeleweka Picha.png Sijui kama nitaeleweka katika hili

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuangalia sura na shepu badala ya vipaji halisi. Kulifanya kuigiza filamu ionekane kitu chepesi. Gonjwa hilo likahamia kwa wanamuziki. Kila msichana mwenye sura na umbo zuri. Akaamini anaweza kuwa bora zaidi ya Jide.

Na mitandao imejenga urafiki nao. Na kumbuka mitandao ya kijamii ina nguvu kuliko wauza unga. Mitandao inaweza kukuhamisha mjini. Kukupora cheo chako. Kukupa ndoa. Kuvunja ndoa. Kukutajirisha. Kukufilisi. Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ugaidi.Na Wabongo wanapenda vitu vyepesi. 

Hawataki vitu vya kufikirisha saana. Na kirusi hiki kimesambaa kwenye vyumba vya wamiliki na ‘stafu’ wa vyombo vya habari. Kuamini kwenye muonekano na sura nzuri, kama kipimo cha ubora wa msanii wa sanaa ya muziki na filamu kwa sasa.

Kila aliye na sura nzuri, anayeweza kuvaa kimini  na kuigiza mambo ya chumbani. Anapewa sifa ya muigizaji bora kuliko Natasha. Au mwanamuziki mkali kuliko Grace Matata na Vumilia. Ndiyo tulipofikia.

Ushindani wa sura na umbo umewatoa nje ya ulingo wa sanaa wenye vipaji. Kama huna muonekano mzuri. Utapewa nafasi ya kuigiza kama mlinzi au taahira.

Wanatulazimisha kuwa mwanaume tajiri ni ‘handsome’. Mke wa tajiri ni mrembo mwenye umbo zuri. Tatizo siyo kuigiza nafasi gani. Ni kwamba hata shavu kwa vyombo vya habari hawapewi.

Sioni tatizo kama Lulu Diva akiigiza na Jb na wakali wengine wa hizi kazi. Huko wanapata muongozo mzuri na hatuoni mapungufu yao. Hujazwa ujasiri na umakini angalau hatuoni mapungufu mengi. Sasa baada ya kila msanii kuwa na kampuni shida ikaanza.

Wasichana ambao kazi yao ilikuwa ni kupendezesha video za wanamuziki. Nao wakawa mastaa wa muziki. Tusubiri kuona Zuchu akifunikwa kwenye tuzo na Hamisa? Ni wakati wa kushindanishwa Nandy na Giggy. Na Giggy kufunika kwa kura nyingi. Ndiyo tunakokwenda.

Baada ya muda tutasikia Faiza Ally ni mkali zaidi ya Yammy au Ruby. Ndicho kilichompoteza Pauline Zongo, kuamini kuwa Snura ni zaidi yake. Ifikie mahala kila mmoja afanye kitu kutokana na uwezo wake. Sanaa iwe na warembo ndiyo, lakini ubora usiwe wa umbo na sura yake.

Yupo ‘Lulu’ Elizabeth Michael. Kaanzia kwenye sanaa ya filamu na urembo wake mpaka leo. Ndivyo ilivyo kwa Johari na Monalisa. Hata Rose Ndauka. Lakini kigezo cha ubora wa msanii isiwe umbo lake na sura.

Tusimtoe mtu huko salon na kuuza duka. Kisa tu ana muonekano na sura nzuri, basi akaingizwa katika zizi la sanaa. Ni upotoshaji wa mchana kweupe. Na ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa soko lao.

Watu hawana wito na sanaa. Maumbo na sura yanalazimisha kuingia kwenye sanaa na siyo utashi wao.Wapo wasanii wa filamu waliopoteza msisimko katika jamii.

Kutokana na soko kushuka, na wengi waliona muziki kama mkombozi. Sometime kichwa kinauma  kusikiliza wimbo wa ‘sista duu’ flan kwa sababu hajui. Ila utapata wapi sehemu ya kusikiliza wimbo wa Vumilia?

Redio na runinga zimekuwa mateka na watu wa aina hii. Na mitandao ya kijamii ndiyo chimbuko lao. Unazi katika muziki unaweza kulifanya soko hili likapauka. Wasanii pia hawaamini katika ubora wa kazi zao. Wanaamini kuwa ukitoka na Dem fulani nyimbo yako itabamba.

Akili hii matope imetokana na umaarufu wa ‘Mondi’ na ‘drama’ zake na Wema. Yes! walipokuwa kwenye lepe zito la mapenzi. Kuna kazi ya kutoa magugu katika filamu sawasawa kazi ya kuondoa takataka kwenye muziki. Wapo wenye ndoto ya kufika mbali kisanii. Na wenye ndoto za ujinga kwa mgongo wa sanaa. Tuwe makini.

Tutafute vipaji halisi na kuviendeleza. Tuifanye sanaa kama kazi za watu walio makini na vipawa halisi. Na siyo kazi za mitindo na warembo. Wauza sura sanaa kwao ni umaarufu na mademu. Wa kike wengi hutumia sanaa kurahisisha njia ya kuwafikia mapedeshee.

Sina tatizo na mtu. Ila kila mtu awe makini aliposimama. Tusiifanye sanaa kuwa kitu cha hovyo. Upuuzi huu ndiyo ulioleta msiba kwenye sanaa ya filamu. Naona kaburi liko jirani sana kwa sababu linachimbwa na vyombo vya habari. Redio, runinga na magazeti. Na kwenye mitandao ya kijamii, ndiko kwenye sumu hatarishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live