Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shtaka la kumpiga Risasi Halyna lafutwa

Alec Baldwin Halyna Hutchins 071024 E0022509316f42f69cefa2d5cbeb60b0 Shtaka la kumpiga Risasi Halyna lafutwa

Sat, 13 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaji Mary Marlowe Sommer ijumaa hii ametupilia mbali shtaka la kuua bila kukusudia dhidi ya Mwigizaji Alec Baldwin katika kifo cha 2021 cha Mwigizaji mwenzake wa sinema, hatua ambayo inamaliza miaka mitatu ya mabishano ya mara kwa mara ya kisheria.

Baldwin alimpiga risasi Mwigizaji mwenzake Halyna Hutchins kwa bahati mbaya wakati wakirekodi seti ya filamu ya “Rust” October 2021, waendesha mashtaka walimshtaki Muigizaji huyo kwa makosa mawili ya kuua bila kukusudia ambayo yote aliyakana.

Mawakili wa Baldwin walikuwa wamewasilisha ombi la kufuta kesi hiyo, wakisema Wapelelezi wa Serikali hawakushiriki ipasavyo na utetezi kwamba Mtu mmoja aliwasilisha sanduku la risasi lililohusishwa na kesi hiyo kwa Wachunguzi.

Jaji Sommer, aliyeongoza kesi hiyo huko Santa Fe, New Mexico, Nchini Marekani amesema risasi zinazoweza kuhusishwa na kifo cha Muigizaji wa sinema Halyna Hutchins ambazo zingeweza kuunga mkono kesi ya Baldwin hazijawasilishwa na Mawakili wake, Polisi na Waendesha mashtaka.

Nyota huyo wa Hollywood ametokwa na machozi baada ya uamuzi huo, kwani kesi hiyo ambayo ilikuwa inaweza kumfanya ahukumiwe kifungo cha miezi 18 ikiwa atapatikana na hatia ilitupwa nje na kuingia katika historia ya matukio ya kustaajabisha kuwahi kujiri katika ulimwengu wa filamu.

Hannah Gutierrez, ambaye alimuandalia silaha hiyo, tayari anatumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa kuua bila kukusudia, Baldwin alikuwa anakabiliwa na shtaka kama hilo, Waendesha mashtaka wanadai alipuuza sheria za msingi za usalama wa bunduki na alitenda kwa uzembe wakati akiigiza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live