Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya uchungaji ya Irene Uwoya

Uwoya Uchungaji Msz Safari ya uchungaji ya Irene Uwoya

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Safari yangu ya Wokovu imeanzia mbali sana, nakumbuka miaka kama kumi iliyopita niliwahi kupokea simu na nilivyopokea hiyo simu, huyo mtu kwenye simu alijitambulisha kama Mchungaji sikumbuki jina lake alikuwa anaitwa nani. Akaniauliza naongea na Ray Kigosi? nikamwambia hapana mimi naitwa Irene.

"Akasema ooh Jesus, akasema aliota yupo stand ya Bus, wakati yupo stand ya Bus alikutana na Ray, wakati yupo na Ray mungu akamwambia kwamba inatakiwa Ray amtumikie, kwahiyo akamuomba Ray namba ya simu. Asubuhi alivyoamka Mungu akamkumbusha tena kuwa mpigie Ray umwambie anatakakiwa kunitumikia.

"Cha ajabu alivyopiga simu nikapokea mimi, yule Mchungaji alishangaa kwanini nimepokea mimi, mimi sikumuelewa lakini akaniambia Mungu anataka umtumikie na ni vyema ukafanya mapema, kiukweli sikumuelewa nikakata simu nilikuwa nimetoka Klub kwenye mambo yangu ya pombe, nilipofika nyumbani nikawakuta ndugu zangu nikawahadithia hawakuniamini, tulipojaribu kupiga tena ile namba haikupatikana mpaka leo.

"Baada ya kumkosa kwenye simu nikaamua kupotezea kwakweli sikutaka hata kujua maana nilikuwa na mambo mengi sana kipindi hicho. Wakati maisha yanaendelea siku moja nilitoka na marafiki zangu wao walikuwa wanasali Mbezi sikumbuki lilikuwa ni kanisa gani, walipomaliza kusali mimi nilikuwa nawasubiri kwenye gari wakaniita nikamsalimie Mchungaji wao.

"Yule Mchungaji akaniambia hivi unajua wewe ni mtumishi wa Mungu? nikasema mimi? Hauwezekani, basi hiyo siku nayo ikapita sikutaka hata kuwaza zaidi nikaona kama naigiziwa sinema tu nikaendelea na maisha yangu ya kawaida.

"Baadae nikawa napata ndoto za maono kuhusu Mungu zaidi, nikaendelea na hiyo hali hadi mwaka jana Mungu alipoongea na mimi ndotoni kwamba nikamtumikie, ndipo nikajua hiki kitu ni siriasi nikaenda mlimani nikafunga siku tatu nikaamua kubadilika na kuianza safari mpya ya utumishi," amesema Irene Uwoya.

View this post on Instagram

A post shared by Irene Uwoya (@ireneuwoya8)





View this post on Instagram

A post shared by Irene Uwoya (@ireneuwoya8)



Chanzo: www.tanzaniaweb.live