Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rushaynah: Manara hana hela!

Video Archive
Wed, 1 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mke wa Haji Manara, Rushaynah amefunguka mengi kumhusu x wake huyo akidaiwa kuwa si kweli kwamba alifuata fedha kwake kwa sababu Manara hana fedha.

Rushaynah amefunguka hayo leo Februari Mosi, 2023 alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari alipokuwa akitangazwa dili lake la ubalozi.

"Haji ana hela?" alihoji baada ya kuulizwa na waandishi kama alifuata hela kwa Haji. Mrembo huyo alisema, Haji ana hela za kawaida lakini si kwamba ana hela kivile.

Mrembo huyo ameweka wazi kuwa mambo yote yanayoendelea katika mitandao ya kijamii ni uongo kwani suala la kumnyima pafyumu halina ukweli wowote na kuongeza kuwa kwa yeyote anayemuona hajatulia aendelee kuamini hivyo kwani hawezi kumuaminisha kila mtu kuwa yeye ni mtulivu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live