Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Rubani kichaa aliyeua watu 150

Ajali Ndege Mdz Rubani kichaa aliyeua watu 150

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hili ni moja ya Tukio baya zaidi na la kukumbukwa katika historia ya Usafiri wa Anga, mnamo Mwezi March 24, 2015 ilionekana kama siku ya kawaida kwa Ndege ya Shirika la Ujerumani (Germanwings Flight 9525) iliyoratibiwa kutoka Barcelona–El Prat Airport nchini Uhispania hadi Düsseldorf Airport nchini Ujerumani.

Kulikuwepo na Marubani wawili, Rubani Patrick na Rubani mwingine Aliyejulikana kwa jina la Andreas Lubitz. Rubani huyo kwa jina la Andreas alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili kwenye Maisha yake ambalo alikuwa akikabiliana nalo kwa kipindi kirefu na marakadhaa alitaka kutoa uhai wake.

Hata Madaktari walithibitisha kuwa kutokana na Matatizo yake hayo hawezi kupewa jukumu la Kurusha ndege na kuwa chini ya uangalizi maalum, lakini hio haikumzuia kutimiza dhamira yake aliyoipanga ambapo alifoji taarifa zake kwenye vipimo na kuonekana amepona tatizo lake kwenye moja ya vipimo

Vipimo viliridhisha kuwa ni mzima hivyo alipewa safari ya Kurusha ndege kama muongozaji mkuu kutokea Uhispania kuelekea Ujerumani na ndege kubwa yenye zaidi ya watu 150.

Muda wa Kunyanyua ndege alimwambia Rubani mwenzake kuwa "Safari itakuwa nzuri na yakupendeza", Rubani mwenzake akamwambia "Natumaini itakuwa hivyo".

Basi ndege ilianza kupasua mawimbi angani ambapo Patrick, Rubani Msaidizi alitoka kwenda Washroom na wakati anarudi alikuta mlango ukiwa umefungwa na Rubani mwenzake Andreas.

Alikuwa na mpango kichwani kwake ambao aliupanga kuutimiza, Alitaka kuyatoa maisha yake wakati huo Rubani mwenzake alijaribu kugonga Lakini hakumfungulia. Aliamuwa kutumia shoka kuvunja mlango Lakini mlango ulikuwa mgumu kuuvunja.

Andreas alikuwa kimya hajibu chochote na kushusha ndege chini hadi kimo cha urefu wa futi 10,000 sawa na Mita 3000, Abiria wote ndani ya ndege walingiwa na woga juu ya tukio hilo.

Kwenye ndege kulikuwa na Wanafunzi 16 na watoto 2 ambao pia walikuwa wakisafiri na ndege hiyo na ndani ya sekunde chache tu ndege hiyo ingegonga Mlima.

Watu wote ndani ya ndege walijawa na hofu kuwa wanaenda kufa na kuanza kusali kumuomba Mwenyezi Mungu, Ndege iligonga Mlima na Abiria wote 144 na wafanyakazi 6 walifariki Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live