Menu ›
Burudani
Sun, 8 Apr 2018
Chanzo: bongo5.com
Leo April 07, 2018 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa mcheza filamu mashuhuri Bongo, Marehemu Steven Kanumba. Wasanii wenzie hawapo nyuma kuenzi yale mazuri aliyofanya katika tasnia hiyo.
Miongoni mwao ni Rose Ndauka ambaye ameeleza kuwa asingefika hapo alipo bila Kanumba. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Tanzania na Dunia itakukumbuka daima , Ushauri wako bado naufatisha. Waswahili husema Rafiki wa kweli sio yule atakae kupa Samaki ukiwa na njaa Bali ni yule atakae kufundisha kuvua samaki ili kesho uweze kukidhi mahitaji yako hata ukiwa mwenyewe piA uweze kuambukiza ujuzi huo wengine.Marehemu Steven Kanumba alifariki April, 07, 2012, kifo chake kilikuwa cha kushtusha na cha ghafla. Alifariki kwa kuanguka chini alipokuwa kwenye ugomvi wa kawaida na mpenzi wake Elizabeth ‘Lulu’ Michael. Kifo chake kilifichua siri ambayo wengi tulikuwa hatufahamu – kwamba Lulu na Kanumba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu.Ulinifunza vyema, nisingekua hapa umekua sababu kubwa ya hapa nilipo. Tutakukumbuka Daima na milele… Rest In Peace Teacher #StevenKanumba #LegendsLiveForever
Chanzo: bongo5.com