Muigizaji maarufu wa Nollywood kutoka nchini Nigeria Ramsey Nouah ambaye kwa sasa yupo Tanzania amesema kuwa anamkumbuka msanii wa Bongo movie marehemu Steven Kanumba kwa sababu ndiye aliyejenga ushirikiano kati Nollywood na Bongo movie.
“Nimemkumbuka Kanumba ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kunileta Tanzania na kushirikiana naye kwenye filamu kadhaa, sitaweza kumsahau alikuwa ni mtu mzuri aliyependa udasisi na kujifunza,” – Ramsey
Ramsey amesema kesho Jumamosi ataenda kutembelea kaburi la Marehemu Kanumba na kuwaomba Watanzania waungane naye.
“Nawaomba Watanzania muungane nami katika kuweka maua na kuwasha mshuma kwenye kaburi la marehemu Kanumba,” – Ramsey
Ramsey na Kanumba waliigiza movie mbili ambazo ni Devils Kingdom na Moses.