Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Live Radio

Afrika

Nchi

Kijamii

Queen Darleen na muziki ndio basi tena

Queen Darleen Queen Darleen

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa kwanza wa kike kutoka WCB, Mwanahawa Abdul Juma maarufu kama Queen Darleen huenda yeye na msanii Vanessa Mdee njia yao ni moja kwani yupo kimya bila kutoa wimbo mpya zaidi ya miaka minne sasa.

Mdau amefunguka kuwa ukimya huu umekuja baada ya Queen kuingia kwenye ndoa ikiwa wimbo wake wa mwisho kuutoa ulikua 'Bachela' aliomshirikisha Lava Lava uliotoka mwaka 2020.

Ukurasa wa instagram wa Queen Darleen una posti moja pekee miaka sasa imepita hana posti..

Mpya lakini bio yake hajaondoa utambulisho wa kuwa bado yuko chini ya Lebo ya WCB inayomilikiwa na kaka yake, Diamond Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live