Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Producer S2kizzy akieleza alivyoingia katika ngoma ya Nikki wa Pili ‘Hesabu’ (+video)

Video Archive
Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Producer kutoka Switch Music Group, S2kizzy amefunguka namna mchakato mzima hadi kuweza kusikika katika ngoma ya Nikki wa Pili ‘Hesabu’ ambayo ameshirikishwa na Joh Makini pia.



S2kizzy ameiambia Bongo5 kuwa baada ya Nikki kufanya verse zake mbili ngoma haikuwa na chorus ndipo Nikki alipomuambia afanye ubunifu wowote kitu ambacho alikifanya na ngoma hiyo kukamilika.

“Kina Joh Makini, Nikki wa Pili ni watu ambao nafanya nao kazi tunashinda wote studio hata ukiangalia combination yetu ni nzuri, ukiangalia kama kwenye ngoma ya Vanessa Mdee na Cassper Nyovest pia itaona pale kuna combination,” amesema.

“Hii ngoma ya Hesabu na Nikki wa Pili katushirikisha mimi na Joh Makini ilikuwa ni Nikki kafanya verse mvili halafu ngoma ilikuwa haina chorus wala Joh Makini alikuwa hajaingiza”

“Nikki alikuwa hajawahi kunisikia nikiimba akaniambia ukiwa na muda wako jaribu kufanya kitu fulani tuangalie itakuwaje, nikafanya nikamtumia akapenda hivyo baada nikafanya serious ikawa imetoka,” ameeleza S2kizzy.

Chanzo: bongo5.com