Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Peter wa P Square apandikiza nywele Uturuki

Peter Hair Transplant.png Peter wa P Square apandikiza nywele Uturuki

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka Nigeria Peter Okoye a.k.a Mr P ameweka wazi kuwa amefanyiwa upasuaji wa kupandikizwa nywele uliyofanyika jijini Istanbul, nchini Uturuki.

Kufuatia na video inayosambaa mitandaoni inaeleza kuwa ameamua kufanya upasuaji huo kutokana na kutopendezwa na muonekano aliyokuwa anao huku akidai kuwa nywele zake zilianza kutoka na kuwa kipara.

Hata hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram alithibitisha kuwa takriban nyuzi 2,400 za nywele zilitolewa kutoka sehemu tofauti ya kichwa chake na kupandikizwa kwenye maeneo yenye upara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live