Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Penzi la Harmonize na Poshy ladaiwa kuvunjika

Penzi La Harmonize Na Poshy Ladaiwa Kuvunjika.jpeg Penzi la Harmonize na Poshy ladaiwa kuvunjika

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna upepo mbaya unaendelea kunako penzi la staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize na mpenzi wake Poshy Queen.

TZW TV imejiridhisha kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ya Instagram ambapo Harmonize amemu-unfollow Poshy Queen na vilevile mrembo huyo amemu-unfollow Konde Boy.

Ishu hii imeibuka ikiwa ni siku chache tu tangu wawili hao waonekane wakiwa pamoja katika uwanja wa Benjamini Mkapa katika tamasha ya Yanga Day.

Je penzi lao ambalo lilikuwa limeanza kukita mizizi tayari limevunjika? Je wawili hao wapo kwenye ugomvi na kufikia hatua ya ku-unfolliana? Tuvute pumzi tutaupata ukweli soon!

Ikumbukwe Poshy aliingia kwenye sintofahamu na DJ wa Harmonize, DJ Seven ambaye alidai kuwa na uhusiano na mrembo huyo lakini hata hivyo Poshy alimkataa.

Baadaye, Seven aliacha kupiga kazi na Harmonize lakini hata hivyo, Seven na Harmonize walionekana Yanga Day wakifanya kazi pamoja.

Harmonize amewahi kuwa kwenye uhusiano na msanii wa filamu nchini Jacqueline Wolper ambaye waliachana na mrembo huyo akaolewa baadaye na Rich Mitindo na kisha baadaye alizama katika penzi zito na muigizaji Kajala Masanja ambaye naye walimwagana.

Hivi karibuni Harmonize alinukuliwa akisema, Poshy ndiyo mwanamke wake wa mwisho na hana mpango wa kuachana na atafunga naye ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live