Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ofisa wa gereza ashtakiwa kwa kulala na mfungwa

DEATHSEX Ofisa wa gereza ashtakiwa kwa kulala na mfungwa

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya habari iliyowashangaza wendi ni pamoja na story kuhusu ofisa wa magereza mwanamke nchini Uingereza kushtakiwa baada ya kupatikana kwa video kwenye mtandao wa kijamii inayodaiwa kumuonyesha akifanya mapenzi na mfungwa katika gereza la HMP Wandsworth, kusini magharibi mwa London, hii ni kuliungana na The Guardian.

Linda De Sousa Abreu, 30, kutoka Fulham, magharibi mwa London, anakabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma na anatarajiwa kufikishwa  Mahakamani.

Polisi wa Metropolitan walianzisha uchunguzi siku ya Ijumaa baada ya video hiyo, inayodaiwa kurekodiwa ndani ya gereza hilo, kusambaa mtandaoni.

“Rushwa ya wafanyikazi haivumiliwi, na afisa wa zamani wa gereza anayedaiwa kuonyeshwa kwenye video hii ameripotiwa kwa polisi,” mwakilishi wa Jeshi la Magereza alisema.

Video hiyo inaripotiwa kuonyesha afisa huyo mwanzoni akiwa amevalia sare kabla ya kujihusisha na kitendo hicho kilichonaswa moja kwa moja.

Ukaguzi wa hivi karibuni ulifunua masuala yanayosumbua, ikiwa ni pamoja na vurugu zilizokithiri, wanyama waharibifu, na changamoto kali za wafanyikazi huko HMP Wandsworth, gereza la enzi ya Victoria lililojengwa mnamo 1851, Kituo hicho, kilichoundwa kwa ajili ya wafungwa wachache zaidi, kwa sasa kinafanya kazi kwa asilimia 163 ya uwezo wake uliokusudiwa, na kinahifadhi zaidi ya wafungwa 1,500 na limekuwa likikabiliana na msongamano mkubwa wa watu na hali mbaya, The Guardian walieleza.

Msemaji wa Scotland Yard alithibitisha uchunguzi kuwaitiske bado unaoendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live