Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka kuwa muziki pendwa huo unaelekea kufa kwani tayari kuna watu ambao wanamamlaka serikalini ambao yeye amewaita wakubwa wana lengo la kuupoteza.
Nay wa Mitego amesema mwaka huu muziki huo utapotea kabisa na wasanii wa muziki huo watapotea kama walivyopotea waigizaji wa Bongo Movie.
Maono ya Nay wa Mitego imekuja baada ya mjadala mzito uliokuwa unarushwa mubashara leo Machi 14, 2018 na kituo cha Clouds FM ambapo Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza na Viongozi wa BASATA walikuwa wanajibu maswali ya wadau na mashabiki wa muziki.
Kwenye mjadala watu wengi waliuliza maswali kuhusiana na vigezo vya kufungiwa kwa wasanii na nyimbo zao huku wengine wakihoji kwanini BASATA wanasimamia kigezo cha maadili pekee? lakini majibu kutoka BASATA hayakuwaridhisha wala kuwaingia vichwani baadhi ya wasanii akiwemo Nikki wa Pili na Rapa Wakazi.
“Kwa mahojiano yao leo mtakua mmeelewa tatizo ni nini.?! Naona mwisho wa huu muziki, Umekwamia hapa rasmi 2018. Mkubwa atabaki kuwa mkubwa na mdogo ataendelea kuwa mdogo. Na tusivyo na umoja tunaenda walikoenda ndugu zetu Bongo Movie,“ameeleza Nay wa Mitego.
Nay wa Mitego ni moja ya wahanga wa adhabu za kufungiwa nyimbo zao na BASATA kwani alishawahi kufungiwa nyimbo kama Wapo, Pale Kati Patamu, na nyingine kibao.
Soma na Hii – BASATA yamfungia Nay wa Mitego kwa muda usiojulikana, akutwa na makosa matatuMwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu Baraza la Sanaa Tanzania kushirikiana na Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia rapa Roma Mkatoliki kutojihusisha na muziki kwa miezi sita huku Nay wa Mitego akipewa onyo kali na serikali kuhusu muziki wake.
Soma zaidi –> Roma Mkatoliki apigwa ‘STOP’ kufanya muziki, Nay wa Mitego apewa onyo kali