Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nandy afunguka mazito ndoa yake ikitimiza miaka miwili

Msanii Nandy Msz Nandy afunguka mazito ndoa yake ikitimiza miaka miwili

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ameamua kufunguka ya moyoni kuhusu mahaba anayopewa na mumewe ambaye pia ni msanii mwenzake, William Lyimo ‘Billnass’ baada ya ndoa yao kufikisha miaka miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nandy amesema ndoa yeke imekuwa fundisho kubwa kwenye maissha yake na kupelekea kujua maana ya upendo.

“Mume wangu miaka miwili ya ndoa yetu imekuwa fundisho kubwa kwangu kujua upendo ni kitu muhimu sana, uwepo wako umerahisisha maisha yangu na ya kipenzi chako NAYA jua tu tunakupenda sana.

Nacho kuomba najua wanaume mmeumbiwa kupepesa macho japo sio mwanaume wangu wewe (joke) popote uendapo, chochote ufanyacho jua una watu wanakupenda na kukuhitaji sana, kuyashinda majaribu now days ni rahisi sababu kila kitu kishapitwa na wakati na wakati wenyewe ndo sasa kuonyesha mfano na kuwa mifano bora kwa watu wenye mapenzi ya kweli kuwa vijana wakiamua inawezekana. MUNGU wangu atulinde nitimize ahadi ya watoto wako 10 NAKUPENDA PY @billnass HAPPY ANNIVERSARY MY LOVE,” amesema Nandy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live