Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nai: Wanaume acheni ubabaifu

Nai Official Nai: Wanaume acheni ubabaifu

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muuza nyago wa video za Bongo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleca, Nairath Ramadhan almaadufu Official Nai anawataka baadhi ya wanaume Bongo kuacha ubabaifu na badala yake wawe wa kweli pale inapotokea wamemuelewa msichana.

Akichezesha taya, Nai anasema kuwa, wanaume wengi siku hizi wamekuwa waongo na waoga kwenye mapenzi, badala ya kumfuata mwanamke na kumwambia moja kwa moja kuwa anamuhitaji, anaanza kujimwambafai kuwa ana pesa wakati hana.

“Yaani siku hizi kuna wanaume wanatia aibu kwa kweli, anamfuata mwanamke na kuanza kujinadi kuwa ana hiki na hiki, halafu mwisho wa siku akishatimiza haja zake, anaanza kumzungusha msichana wa watu.

“Sikilizeni kama umempenda mtu ni bora umwambie ukweli ili na yeye akufikirie, lakini siyo kujinadi kuwa utamfanyia mambo f’lani, halafu mwisho wa siku unaingia mitini, huu ni ubabaishaji mkubwa wanaume baadhi yenu wenye tabia hii mnatakiwa kuiacha mara moja,” anasema Nai ambaye ngoma yake ya Siyo Saizi Yako bado inabamba mashabiki wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live