Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Yusuph amuwashia moto Diamond, baada ya kukataa tuzo (Video)

Video Archive
Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme wa muziki wa Taarab Mzee Yusuph ambaye ni kiongozi katika Shirikisho la Muziki Tanzania, amewasha moto kujibu kauli kuhusu tuzo za muziki ya Msanii Diamond Platnumz ambayo aliitoa hivi karibuni akihojiwa na Wasafi Fm kuhusu tuzo za muziki nchini Tanzania.

Mzee Yusuph amezungumza hayo muda mfupi baada ya kumtangaza Steve Nyerere kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania.

Wiki hii Diamond alinukuliwa na vyombo vya habari akikataa kushiriki kwenye tuzo hizo kwa kukosa imani na jinsi zilivyoandaliwa.

“Kama hujaweza kunipa mirabaha utanipa tuzo? Unazungumzia tuzo zinazokuja wadau aliokuwepo katika tuzo ni wadau kutoka kwenye vyombo vya habari. Hawapigi nyimbo zangu watanipa mimi tuzo,” aliongea Diamond kupitia The Switch ya Wasafi Fm.

Aliongeza, “Kwangu Mimi YouTube naona inanitosha, Lakini tuzo zinafaa kwa wasanii wengine nchini Tanzania. Lakini mimi focus yangu binafsi na focus kupambana na watu wa nje ya Tanzania kuleta heshima Tanzania. Ukiniweka nashindana na msanii wa Tanzania ni kwenda kumkandamiza kwa sasabu hatoniweza kwa sabubu mimi nina vigezo vingi vyakufanya vizuri, kwanza nakipaji, na uwezo wa bajeti ya promotion, nacheza, mnyamwezi,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live