Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwanamke aliyepotea apatikana akiwa amemezwa na chatu

Chatuuuuuu (4).jpeg Mwanamke aliyepotea apatikana akiwa amemezwa na chatu

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke aliyetoweka, amepatikana akiwa kamezwa mzima na chatu mkubwa baada ya wenyeji kumkata tumboni mwa nyoka huyo.

Mama wa watoto wanne Farida, 50, alitoweka alipokuwa akipita kwenye pori kwenda kuuza chakula katika soko la karibu na nyumbani kwake katika kijiji cha Kalempang, Indonesia, Juni 6.

Chatu huyo alitumbukiza meno yake kwenye mguu wake huku akizunguka mwilini mwake na kumkaba kabla ya kuanza kumeza kichwa chake kwanza.

Mume wa Farida Noni, 55, aliingiwa na wasiwasi baada ya kuona mkewe hajarejea nyumbani hadi usiku na kuwatahadharisha wenyeji wengine ambao walianza kutafuta.

Walimkuta chatu mkubwa mwenye urefu wa futi 20 akiwa amejitanda kwenye kichaka siku iliyofuata, akiwa na uvimbe mkubwa tumboni. Kichwa chake kikubwa, kinaonekana kwenye video kutoka eneo la tukio, huku ulimi wake akiupeperusha kutoka kwenye midomo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live