Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwaitege: Mimi sijafa, ni mzima wa afya njema

Bonny Mwaitege Msz Bonny Mwaitege.

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege amesikitishwa na taarifa za watu katika mitandao ya kijamii wanaomzushia kifo.

Akizungumza nasi leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema kuwa yeye ni mzima wa afya na amesikitishwa na uzushi huo unaosambazwa mitandaoni.

"Aise pole sana dada yangu, mimi ni mzima wa afya njema wala sijafa. Huu uzushi tu wa watu ukweli nimesikitika sana, maana nimeanza kupigiwa simu na watu kutokea Nairobi na Dar na mikoa mingine, hii ni mbaya sana. Hapa sasa hivi nipo njiani naelekea Nairobi kwenye kazi za injili, Mungu ni Mwema," amesema Mwaitege.

Alipoulizwa iwapo uzushi huo kuwa ametengeneza kiki, amesema sio kiki kwani kwa hatua aliyopo sio wa kutaka kufanya kitu atumie kiki.

"Kwa nini nifanye kiki? Yaani kiki ndio nijiue mwenyewe? Kwa hatua niliyofikia ya kazi ya sanaa yangu sio ya kufanya kiki ndio nifanye kitu," amesema Mwaitege.

Mwimbaji huyo amewahi kutamba na nyimbo nyingi zikiwemo Safari Bado, Dunia Dunia, Acha Nizaliwe, Bado Nampenda, Mke Mwema, Sisi Sote, Imba, Mama na Neema Imenibeba na nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live