Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Music Facts: Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Dogo Janja (+video)

Video Archive
Sat, 17 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Wiki iliyopita tulikuleta mambo 10 kuhusu Rayvanny wa WCB, leo ni zamu ya Dogo Janja kutoka Tip Top Connection.



Kupitia Music Fats ya Bongo5 tunakuletea mambo 10 ya kawaida kabisa kuhusu Dogo Janja lakini si rahisi kuyabaini.

1. Ngoma pekee ya Dogo Janja kufanyiwa remix ni My Life, remix ya ngoma hiyo aliwashirikisha Radio na Weasel ambao walikuwa wanaunda kundi la Goodlyfe.

2. Video ya harusi ya Dogo Janja na Irene Uwoya imetazamwa zaidi kuliko video za nyimbo zake zote katika channel yake ya YouTube, video hiyo ina views milioni 1.5.

3. Tangu kurudi upya katika muziki mwaka 2016, Dogo Janja katika video zake nne alizotoa tatu zimeongozwa na ma-director waliowahi kushinda tuzo za Watu, Hanscana aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2015 ameongoza video mbili ‘My life na Kidebe’, wakati Nisher aliyeshinda mwaka 2014 ameongoza video moja ‘Wayu Wayu’.

4. Kwa taarifa yako kuna kolabo kati ya Dogo Aslay na Dogo Janja iliyojulikana kwa jina la Nimeshamaliza, ila hakuna kolabo kati ya Aslay na Dogo Janja. Usichanganyikiwe hapo tofauti ni majina tu.

5. Tangu mwaka 2016 katika ngoma nne alizotoa Dogo Janja hajamshirikisha msanii yeyote katika ngoma zake, pia ni wasanii wawili tu waliomshirikisha katika ngoma zao ambao ni Casso na Chindo Man.

6. Kuna video mbili tu ambazo Dogo Janja ametokea akiwa amevaa sare za shule, video hizo zote zilitoka mwaka 2012, video ya kwanza ni ‘Shikamoo Mwalimu’ aliyoshirikishwa na Easy Muchwa na video ya pili ni Kusoma aliyoshirikishwa na Dogo Sheby.

7. Licha ya kukaa ndani ya familia ya Tip Top Connection kwa kipindi kirefu, Dogo Janja hajawahi kusisikaka katika ngoma yoyote iliyowakutanisha wasanii wa Tip Top Connection kama kundi.

8. MJ Records ndio studio ambayo Dogo Janja amefanya nyimbo nyingi zaidi tangu alipoanza muziki, nyimbo alizotoa hapo ni kama Siri Zao, Mtoto wa Uswazi, Yamoyoni, My Life, Kidebe, Ukivaaje Unapendeza? na Wayu Wayu sawa na zaidi ya asilimia 70 ya nyimbo alizotoa.

9. Wimbo wa Dogo Janja ndio ‘Ngarenaro’ ndio wimbo wa kwanza kutoka katika studio ya Rayvanny inayofahamika kama Surprise Music.

10. Dogo Janja ameanza kuvaa miwani katika video zake mwaka 2016 alipotoa ngoma ‘My Life’ na amefanya hivyo hata katika ngoma alizoshirikishwa, kabla ya mwaka huo hakuna video yoyote aliyotokea akiwa na miwani.

Chanzo: bongo5.com