Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshiriki 'Miss South Africa' ajiondoa kufuatia utata wa uraia wake

Chidimma Adetshina.jpeg Chidimma Adetshina

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo anayeshiriki shindano la Miss South Africa amejiondoa kwenye shindano hilo, akisema amechukua uamuzi huo kwa ajili ya usalama na ustawi wa familia yake.

Tangazo la Chidimma Adetshina kwenye ukurasa wake wa Instagram limekuja siku moja baada ya uchunguzi wa awali wa wizara ya masuala ya ndani kubaini kuwa mama yake huenda alihusika katika ‘kuiba kitambulisho’ ili kuwa raia wa Afrika Kusini.

Bi Adetshina mwanafunzi wa sheria mwenye umri wa miaka 23 amesema alizaliwa Soweto, kitongoji kilicho karibu na Johannesburg, na alikulia Cape Town.

Katika mahojiano na vyombo vya habari alieleza kuwa baba yake alikuwa Mnigeria na mama yake alikuwa Mwafrika Kusini mwenye asili ya Msumbiji.

Kwa wiki kadhaa, mjadala kuhusu asili yake ulizua gumzo katika mitandao ya kijamii, huku baadhi ya Waafrika Kusini wakijiuliza ikiwa alikuwa raia wa Afrika Kusini.

Kadri mijadala ilivyozidi kuongezeka, waandaaji wa shindano la Miss South Africa waliomba wizara ya mambo ya ndani kufanya uchunguzi kabla ya tukio la Jumamosi.

Katika taarifa yake idara ya mambo ya ndani ilisema imegundua kuwa mama yake na Adetshina huenda aliiba kitambulisho mtu mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live