Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mshawishi wa Instagram afungwa jela kwa ulanguzi na utumwa

Mshawishi Wa Instagram Afungwa Jela Kwa Ulanguzi Na Utumwa.png Mshawishi wa Instagram afungwa jela kwa ulanguzi na utumwa

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: Bbc

akati wasichana wawili wa Kibrazili waliporipotiwa kutoweka mnamo Septemba 2022, familia zao na Shirika la Upelelezi la Marekani – FBI, walianzisha msako mkali kote Marekani ili kuwapata. Walichojua ni kwamba walikuwa wakiishi na mshawishi wa Instagram Kat Torres.

Torres sasa amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa ulanguzi wa binadamu na utumwa wa mmoja wa wanawake hao.

BBC pia imeambiwa kuwa mashtaka yamewasilishwa dhidi yake kuhusiana na mwanamke wa pili.

Je, mwanamitindo huyo wa zamani ambaye aliwekwa kwenye jalada la magazeti ya kimataifa alianzaje kuwahadaa wafuasi wake na kuwarubuni katika ulanguzi wa kingono?

"Alikuwa kama mwenye kunipa tumaini," anasema Ana, akielezea hisia zake baada ya kuona ukurasa wa Instagram wa Torres mnamo 2017.

Ana hakuwa mmoja wa wanawake waliopotea waliolengwa katika msako wa FBI - lakini yeye pia alikuwa mwathirika wa kulazimishwa na Torres na angekuwa muhimu kwa uokoaji wao.

Anasema alivutiwa na historia ya Torres kutoka kuwa mtu masikini wa Kibrazili hadi mwanamitindo wa kimataifa, akishirikiana na waigizaji mashuhuri wa Hollywood.

"Alionekana kama alikuwa ameshinda ghasia katika utoto wake, unyanyasaji, matukio yote ya kutisha," Ana aliambia Uchunguzi wa BBC Eye na BBC News Brasil.

Ana mwenyewe alikuwa katika mazingira magumu. Anasema aliteseka utotoni kwa vurugu, alihamia Marekani peke yake kutoka kusini mwa Brazili, na awali alikuwa katika uhusiano wa unyanyasaji.

Torres alikuwa amechapisha hivi majuzi wasifu wake uitwao A Voz [The Voice], ambamo alidai kuwa angeweza kutabiri kutokana na nguvu zake za kiroho, na alikuwa amehojiwa kwenye vyombo vya habari maarufu vya Brazili.

“Alikuwa kwenye jalada la magazeti. Alionekana na watu maarufu kama vile Leonardo DiCaprio. Kila kitu nilichoona kilionekana kuwa cha kuaminika, "anasema.

Ana anasema alivutiwa hasa na mtazamo wa Torres wa kiroho.

Kitu ambacho Ana hakujua ni kwamba simulizi ya kutia moyo aliyosimulia Torres ilitokana na nusu ukweli na uwongo.

Chanzo: Bbc