Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii afariki kwa ajali ya moto

Arcella Uwizera Fd Msanii afariki kwa ajali ya moto

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mwamuzi wa soka wa kike nchini Burundi, Arcella Uwizera amefariki dunia katika ajali ya moto mkali iliyotokea Jumanne wiki hii Wilaya ya Nyalukemba huko Bukavu, DR Congo, baada ukumbi wa starehe alipokuwa anafanyia kazi kuteketea kwa moto.

Nyumba tano za makazi pia ziliteketea kwa moto. Kwa mujibu wa taarifa, watu wawili ndio waliofariki Dunia ambao ni pamoja na Arcella ambaye ni Mrundi na Mnyarwanda ambao walikuwa wakihudumu katika ukumbi huo (bar).

Ajali hizi za moto zinakua kama desturi huko Bukavu ambapo siku moja kabla watu watatu walikufa katika ajali nyingine ya moto maeneo ya Panzi na Cimpunda na kufikisha jumla ya matukio 81 ya moto huko Bukavu tangu Juni mwaka huu.

Nyumba hizo zimekuwa zikichomwa moto na watu wasiojulikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live