Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii Yago akimbia nchi

Yago Pon Dat Yago Pon Dat

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa idara ya ujasusi nchini Rwanda, Dr. Murangira Thierry ametangaza kuwa mwandishi na mwanamziki maarufu nchini humo Nyarwaya Innocent anayejulikana kama Yago Pon Dat aliikimbia nchi baada ya kushutumiwa kwa makosa mazito.

Yago alitangaza kuikimbia Rwanda baada ya kutangaza katika mitandao ya kijamii kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakimtafuta kwa ajili ya kumuua.

Agosti 31,2024 aliweka video kwenye mtandao wa kijamii na kuweka orodha ndefu ya watu ambao wamekuwa katika migogoro wakiwemo waandishi wa habari,wasani na watu wengine maarufu.

Katika mkutano na waandishi wa habari,DR Murangira amefahamisha kuwa mwanamziki huyo aliitoroka nchi baada ya kuanza kutafutwa na maafisa wa upelelezi kwa shutuma za kuleta ubaguzi wa kikabila nchini Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live