Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mrembo aliyedai kufanya mapenzi na nyoka aomba radhi

Video Archive
Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima, alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.

Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.

Jana 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.

“Mimi ni yule binti niliyefanya interview nikadai huwa ninafanya mapenzi na nyoka, nikiri ile haikuwa kweli, ninaomba radhi kwa Watanzania wote na Serrikali ya Muungano wa Tanzania niweze kusamehewa.

“Nilitumia maneno ambayo yako kinyume na maadili ya Kitanzania, ninaomba radhi sana kwa sababu mimi sifanyi mapenzi na nyoka. Niliongea vile kwa nikiamini ni sanaa kumbe ninakwenda kupotosha watoto wadogo, watu wazima na wengine, naomba Watanzania mnisamehe sana,” amesema binti huyo.

Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.

Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live