Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr Blue kafikisha kolabo 1000, akataa kuitwa legendary

Video Archive
Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: Bongo5

Msanii wa muziki wa Bongo Flavour, Heri Samir "Mr blue" Ijumaa hii amezungumza na waandishi wa habari wakati akim-support msanii mpya wa Singeli, Elisha kutoka lebo ya boss kapaka Entertainment ambapo rapa huyo alipata kufunguka mengi kuhusu muziki wa BongoFleva.

Rapa huyo amesema yeye ni msanii ambaye amefanya kolabo nyingi zaidi ambapo amedai mpaka sasa amefanya zaidi ya kolabo 1000 za wasanii tofauti tofauti, wakubwa kwa wadogo.

Amesema amekuwa akifanya hivyo ili kuibua na kuwapa nafasi wasanii wapya wenye vipaji huku akimtolea mfano msanii wa Singeli dogo elisha ambaye ameachia naye kolabo ya pamoja ya wimbo, Unanikosha remix.

Chanzo: Bongo5