Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mke wa Sadio Mane arudi shule

Mane Ndoa Mke wa Sadio Mane arudi shule

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kati ya habari zilizoteka vichwa vya habari wiki hii ni ya mchezaji wa timu ya Senegal, Sadio Mane kufunga ndoa na Aisha Tamba.

Ndoa hiyo ilifungwa Januari 7, 2024  huko Keur Massar, kitongoji cha mji mkuu wa Dakar, siku kadhaa kabla ya kuanza kwa Kombe la Afrika (AFCON) 2023.

Hata hivyo mke huyo wa  Mane, mwenye  miaka 19,  ni mwanafunzi, hivyo baada ya kumaliza sherehe za ndoa amerejea shuleni anaposoma na kupokewa kwa shangwe na nderemo na wanafunzi wenzake.

Katika mapokezi hayo, Aisha aliyokuwa juu ya ghorofa akiwa amevalia hijabu nyeupe na sare za shule, alionekana kufurahia mapokezi hayo kutoka kwa wanafunzi wenzake hadi kuonyesha dalili za kutaka kulia.

Kama ndoa ilivyofungwa kimyakimya, ndivyo fungate baina ya wawili litakavyokuwa, tayari Mane na wachezaji wenzake wa timu ya taifa wameshaondoka nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya AFCON, hivyo itamlazimu Aisha kumsubiri mumewe kwa takribani siku 28 mashindano hayo yatakapohitimishwa.

Taarifa ni  kwamba wawili hawa walianza kuwa na uhusiano miaka miwili iliyopita, wakati huo Aisha akiwa na miaka 17. Kulingana na sheria za Senegal mtoto wa kike anaruhusiwa kuolewa pindi atakapofikisha miaka 16, hivyo alichokifanya Mane kuwa na uhusiano na kigoli huyo hajavunja sheria yoyote.

Tovuti ya Pulsesport ya nchini humo imeandika kuwa katika kipindi chote ambacho binti huyo anasoma, Mane aligharamia mahitaji yake ya shule kuhakikisha anapata elimu bora na hata sasa baada ya kumuoa bado atajiendeleza kielimu.

Katika mahojiano ambayo amewahi kufanya Mane mwaka 2022, alieleza mke atakayemuoa ni lazima awe anamuheshimu Mungu na anayesali.

“Naona watu wengi wananiuliza kwa nini sijaoa, mwanamke nitakayemuoa hawezi kuwa kwenye mitandao ya kijamii. Ni lazima awe mcha Mungu na mwenye kusali, hivyo kila mtu ana uchaguzi wake inapofikia kwenye suala la mapenzi,” alisema Mane.

Kabla ya ndoa hiyo kufungwa hakukuwa na taarifa za Mane kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yeyote na hata kama alikuwa basi alifanya kwa siri kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live