Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mimi Mars kiroho safi kwa Marioo

Mars Marioo Mimi Mars kiroho safi kwa Marioo

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa filamu na muziki nchini, Mimi Mars amesema hana kinyongo na aliyewahi kuwa mchumba wake, Marioo katika uhusiano mpya alionao kwa sasa zaidi ya kumtakia kila la kheri.

Mimi Mars aliliambia Mwanaspoti juu ya ukimya wake na Marioo tangu watemane ni kwa sababu hana tatizo na zilipendwa wake huyo ambaye kwa sasa ana uhusiano na Paula na amezaa naye mtoto.

"Nadhani niseme tu, mimi nilikuwa kimya sababu ya ajali niliyoipata, ndiyo maana hata katika tamthilia ya Jua Kali nafasi yangu ilichukuliwa na Elizabeth Michael 'Lulu', kuhusu Marioo kupata familia namtakia maisha mema na familia yake mpya," alisema Mimi Mars aliyeibukia tamthilia ya Jiya.

Marioo na Mimi Mars waliwahi kuwa wachumba, lakini ghafla upepo ulibadilika na kila mmoja kushika lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live