Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka 10 bila Steven Charles Kanumba

Kanumba 10.jpeg Steven Kanumba

Thu, 7 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Aprli 7, 2022 imetimia miaka 10 tangu kifo cha muigizaji wa Bongo Movies Steven Charles Kanumba aliyefariki Aprili 7, 2012. Kanumba atakumbukwa kwa mapinduzi makubwa aliyowahi kufanya katika tasnia ya filamu hapa nchini.

Diamond Platnumz katika moja ya nyimbo zake inayofahamika kama “nawaza” iliyopo katika EP yake ya FOA inayoendelea kufanya vizuri sana Afrika mashariki, moja ya mashairi yaliyopo katika wimbo huu yaliyogusa mioyo ya wapenzi wa bongo movie na watanzania kwa ujumla ni pale Diamond alipoimba au kusema hivi “ nawaza huwenda Steven Kanumba angelikuwepo hai movie zetu pia tungejidai”.

Wimbo huo umefanya vizuri sana kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo youtube na kuibua hisia nyingi kwa mashabiki na wapenzi wa filamu hapa nchini.

Leo Kanumba anatimiza miaka 10 tangu afariki dunia, unadhani nini kifanyike ili kumuenzi mwanamapinduzi huyu wa filamu hapa nchini? Nini mawazo yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live