Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mdee: Nipo singo na sina mtoto

Mdee Pic Mdee: Nipo singo na sina mtoto

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee (Chadema) amefunguka kuhusu maisha yake binafsi akisema kwa sasa yupo single (hana mahusiano) wala mtoto kwa sababu bado hajajaliwa kupata mtoto.

Mdee amesema hayo akihojiwa na Wasafi TV na kusema kuwa wakati amehitimu masomo na kuanza kazi hakutaka kabisa kuwa mwanasiasa kwa sababu alikua akiwaangalia wanasiasa hawaleweki na ni wajanja wajanja sana.

Aidha, Mdee amesema kuwa sasa yupo likizo (nje ya Operation za Chama) kutokana na Kesi ya kufukuzwa uachama wa Chadema, lakini anazi-miss harakati, "unachaaje kuzi-miss harakati wkati umekullia katika hayo mambo?"

Mdee ameongeza pia kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ana mchango mkubwa sana kwake kisiasa kwani aliwachukua yeye na Zitto Kabwe wakiwa wadogo na kuwashika mkono kuwaingiza kwenye siasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: