Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandojo kuzikwa Singida

Mandojo Domokaya Mandojo kuzikwa Singida

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongofleva Mandojo amefariki dunia jana Jumapili, Agosti 11 2024, akiwa Jijini Dodoma.

Msanii mwenzake aliyefanya naye kazi kwa ukaribu Domokaya na Soggdoggyanter wamethibitisha taarifa hiyo ya kifo cha Mandojo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali Mandojo amefariki kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi baada ya kutokea mtafaruku kati yake na mtu mmoja ambaye alimuitia mwizi.

"Kwa sasa msiba upo Dodoma lakini kwa mujibu wa mdogo wake Yohana Chacha anasema mazishi yatafanyika Manyoni, Singida sehemu ambapo amekulia Mandojo"

"Kesho inawezekana ikafanyika taratibu za kusafirisha. Taarifa za kifo nimezipata nikiwa Dar es Salaam" - anasema Domokaya kuhusu kifo cha rafiki yake Mandojo

Miongoni mwa ngoma za Mandojo;

1. Nikupe nini - Mandojo & Domokaya 2. Wanoknok - Mandojo & Domokaya ft. Jaydee 3. Taswira - Mandojo & Domokaya ft. J. Nature 4. Kaunta ya Juu - Mandojo & Domokaya 5. Dingi - Mandojo & Domokaya 6. Kazi yake Mmola - Madee ft Mandojo & Dodmokaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live