Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandojo auawa kwa kupigwa akidhaniwa kuwa ni mwizi

Mandojo 6174205.jpeg Mandojo auawa kwa kupigwa akidhaniwa kuwa ni mwizi

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva nchini, Mandojo amefariki dunia asubuhi ya jana Agosti 11, 2024 jijini Dodoma.

Msanii mwenzake na rafiki yake wa karibu ambaye pia ni msanii, Domokaya amethibitisha kutokea kwa msiba huo ambapo ameeleza kuwa bado hajafahamu chanzo cha kifo cha swahiba wake huyo.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, zimeeleza kuwa Mandojo amefariki dunia kwa kupigwa na wananchi waliodhani kuwa ni mwizi.

Inaelezwa kuwa Mandojo alikuwa baa ambapo kulitokea kutoelewana kati yake na watu aliokuwa nao, ambao baadaye walimuitia mwizi na kusababisha wananchi kujaa na kuanza kumshambulia, wakidhani ni mwizi.

Baadaye aliokolewa na wasamaria wema na kupelekwa hospitali ambako alifikwa na mauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya alipotafutwa, simu yake imepokelewa na msaidizi wake ambaye amesema bado taarifa hizo hazijamfikia na kwamba Jeshi la Polisi linafuatilia na litatoa taarifa kamili baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live