Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madai ya unyanyasaji wa kijinsia yatikisa tasnia ya filamu ya India

Madai Ya Unyanyasaji Wa Kijinsia Yatikisa Tasnia Ya Filamu Ya India.png Madai ya unyanyasaji wa kijinsia yatikisa tasnia ya filamu ya India

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Maneno ambayo yamekuwa yakigonga vichwa vya habari na kutikisa tasnia yenye shughuli nyingi ya filamu katika jimbo la Kerala kusini mwa India tangu wiki iliyopita yamekuwa ni madai, maafisa kujiuzulu na malalamiko ya polisi.

Jimbo hilo limekuwa likishuhudia msururu wa madai ya unyanyasaji wa kijinsia kwa baadhi ya nyota wa kiume tangu ripoti ya kihistoria iliyoangazia shida zinazowakabili wanawake katika tasnia hiyo kutolewa wiki iliyopita.

Sekta hii, ambayo hutengeneza takribani filamu 150-200 za lugha ya Kimalayalam kwa mwaka, ni biashara muhimu, iliyochangamka ambayo imetengeneza baadhi ya sinema zenye sifa kuu na zinazoendelea kuibuka kutoka India.

Lakini ripoti hiyo ya kurasa 290 ya jopo la wanachama watatu - inayoitwa kamati ya Hema - ilielezea kwa kina matatizo yanayowakabili wanawake katika sinema ya Kimalayalam, ikiwa ni pamoja na mazingira duni ya kazi na unyanyasaji wa kijinsia uliokithiri.

Chanzo: Bbc