Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa video hii, Dogo Janja ni Mbunifu, Bahili au Kiki?

Video Archive
Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Kitu kipya kwa sasa kutoka familia ya Tip Top Connection ni video mpya ya Dogo Janja ‘Wayu Wayu’ iliyotoka usiku wa kuamkia leo.



Kabla ya watu kufahamu kilichoimbwa katika wimbo huo, video yake ndio imekuwa mjadala kila mahali baada ya Dogo Janja kuoneka akiwa na muonekano wa kike.

Kabla hata ya video yenyewe kutoka cover ya wimbo nayo iliashiria kitu kama hicho lakini maudhui ya wimbo hayakutoa majibu ya moja kwa moja hadi pale video ilipotoka.

Kama ilivyooneka katika video Dogo Janja anaoneka akiwa amecheza nafasi ya video queen, muhudumu wa mgahawa, mlinzi wa getini na akijivika ule uhusika wa msanii mwenye wimbo.

Kitu kama hiki ni kigeni katika video za Bongo Flava ila katika video za wachekeshaji kama Joti na Eric Omondi ni kitu cha kawaida kutokana wao ni waigizaji na sio waimbaji.

Sasa baada ya video hiyo iliyoongozwa na Nisher kuonekana mashabiki wamekuwa na maoni tofauti tofauti.

Wengine wakidai ni ubunifu katika sanaa, wengine wakieleza kama Dogo Janja kaamua kuweka fedha ya video queen mfukoni na wengine ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa anatafuta attention (kiki) ya muziki wake.

Maoni ya Mashabiki Mtandaoni

  • princesstalha96Ahahahha janjaro ntakupasua unajua… hahahah nimecheka kwa saut
  • dianalazaro99Yan ilikua ubahili wa kuchukua video queen au ndo unatangaza Biashara weye
  • mamuu.mamuu.96Acha nikuambie ukweli nilikuwa najivunia ww nimsaanii unaetuwakilisha chuga kumbe unatamani kuwa shoga washaanza kukupakua hiyo videos wala sioyakuangalia kwamtu mwenye akili timamu
  • bob_sule47@saybmamy_swirry hahahaha Noma hun but umeielewa idea yake
Chanzo: bongo5.com