Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kutana na Jamii ya watu wenye vidole viwili vya miguu

Jamii Vidole Viwili Kutana na Jamii ya watu wenye vidole viwili vya miguu

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa hali ya kawaida Binadamu ana vidole vitano mguuni, lakini kuna baadhi ya watu ambao huzaliwa wakiwa wana vidole pungufu.

Nchi ya Zimbabwe kuna kabila linaitwa Vadoma, kabila hili hupatikana Kanyemba, Kaskazini mwa Zimbabwe, watu wengi kwenye jamii/kabila hilo wana vidole viwili, kwa upande wao huona kama ni baraka kutoka kwa Mungu kwani vidole hivyo huwasaidia kupanda miti kwa uharaka zaidi kwa ajili ya kujitafutia matunda na vyakula vinginevyo.

Kwa Kitaalamu tatizo hili linaitwa "Ectrodactyly", ni tatizo la kurithi (Genetics), tatizo haliishi kwenye jamii hiyo kwa sababu miongoni mwao ni kosa kubwa kuoa nje ya jamii yao, kwahiyo huoana wao kwa wao, hali inayosababisha hata vizazi vyao miguu iwe ina vidole viwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live