Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kupima DNA hewani kunaweza kupunguza bei ya chakula - utafiti

Kupima DNA Hewani Kunaweza Kupunguza Bei Ya Chakula   Utafiti.png Kupima DNA hewani kunaweza kupunguza bei ya chakula - utafiti

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Wanasayansi wanaochukua sampuli za DNA angani kufuatilia kuenea kwa magonjwa hatari wanasema kazi yao inaweza kusaidia kufanya bei za vyakula kuwa nafuu.

Taasisi ya Earlham ilisema michakato yake ya sampuli ya hewa hugundua bakteria, virusi na viumbe vidogo vidogo - ambavyo vinatishia mimea, wanyama na wanadamu - haraka na kwa usahihi zaidi kuliko mbinu zingine.

Hii inaweza kusaidia wakulima kukuza mazao kwa bei nafuu na kwa ufanisi zaidi kwani hawangehitaji kutumia kemikali nyingi. Inaweza pia kubadilisha kazi ya uhifadhi wa mazingira pamoja na hatua za afya ya umma.

Viumbe vyote vilivyo hai vinaendelea kumwaga vipande vya DNA kwenye mazingira yao.

Mia Berelson, ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika taasisi hiyo, anasema mbinu hii inatupa wazo la nini kinaishi wapi, lini, kwa haraka sana.

"Kila kifaa hufanya kazi maalum na huvuta zaidi ya lita 200 za hewa kwa dakika," anasema.

"Hewa hupitia kwenye kichungi, na chochote kilicho hewani - kama vile viini vya bakteria, seli za ngozi, chembechembe tofauti - ambazo hukwama kwenye chujio."

DNA hiyo itapangwa na wasifu utaundwa wa viumbe vyote tofauti vilivyogunduliwa katika eneo hilo.

Taasisi ya Earlham imekuwa ikitoa sampuli za hali ya hewa karibu na mashamba ya wakulima kwa miaka kadhaa lakini sasa pia inachukua sampuli za maeneo ya pwani, misitu na miji pia.

Chanzo: Bbc