Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe Baba Levo na Harmonize fresh kabisa!

Harmonize Ataka Kuzichapa Na Baba Levo.png Baba Levo na Harmonize

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva na Chawa Promax wa Diamond Platnumz, Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo amesema kuwa yeye hana chuki wala bifu na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize ambaye aliwahi kuwa chini ya Lebo ya WCB.

Baba Levo ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi Media amesema kuwa yeye amekuwa akisema mambo ambayo ni chanya kwa Harmonize na kama yakifanyiwa kazi basi msanii huyo anaweza kufanya vizuri zaidi.

"Chuki ambayo watu wanaweza kufikiria kwamba harmonize ananichukia mimi inakuwa ni tofauti kwa sababu mimi nikiongea kuhusu Harmonize yeye mwenyewe akisikia anasema huyu jamaa yuko sahihi na anaongea facts.

"Kama kipindi kile cha tuzo nilisema nyimbo zake ambazo zinatakiwa ziingie kwenye vipengele. Walimwekea nyimbo ambazo kiuhalisia hazina nguvu ya kupambana na ngoma ambazo zipo kwenye mashindano wakati yeye anazo ngoma ambazo zina nguvu na zingeleta ushindani, kwa hiyo iko hivyo," amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: