Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kizimbani kisa kutomtibu mtoto kwa wakiamini maombi

Elizabeth Struhs Kizimbani kisa kutomtibu mtoto kwa wakiamini maombi

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washirika wa kundi la kidini Nchini Australia wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kumuua Binti aitwaye Elizabeth Struhs mwenye umri wa miaka nane mwenye kisukari kwa kumnyima matibabu na badala yake kusali wakiamini kuwa Mungu atamponya.

Elizabeth alikutwa akiwa amefariki katika nyumba moja huko Toowoomba karibu kilomita 125 Magharibi mwa Brisbane January 2022, baada ya kudaiwa kutokuwa na insulini kwa siku kadhaa bila matibabu.

Waendesha mashtaka wanasema kikundi hicho kilikwepa matumizi ya dawa na kumwamini Mungu kumponya Mtoto huyo imani kali ambazo tayari zilikuwa zimemaliza maisha ya Elizabeth katika hali kama hiyo miaka mitatu kabla.

Wazazi wa Msichana huyo ni miongoni mwa Washtakiwa 14, ambao wote wamekataa Mawawili pia wote wamechagua kutojibu mashtaka yoyote, hata hivyo Mahakama inazingatia kwamba ombi la kutokuwa na hatia litazingatiwa.

Mama wa Msichana huyo, Kerrie Struhs(49), Kaka wa Msichana Zachary Struhs (21), na wengine kumi wenye umri wa miaka 22 hadi 67 wanatuhumiwa kwa mauaji, kutokana na utata na kujulikana kwa kesi hiyo ambayo inatarajiwa kudumu kwa karibu miezi mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live