Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kipato, msongo wa mawazo chanzo cha migogoro ya familia

Tatizo La Msongo Wa Mawazo Na Namna Ya Kupekana Nalo Kipato, msongo wa mawazo chanzo cha migogoro ya familia

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipato, msongo wa mawazo, malezi na kukosekana kwa elimu ya ndoa vimetajwa kuwa sababu za mifarakano inayosababisha kuvunjika au kuwapo kwa familia nyingi zenye migogoro.

Tanzania leo inaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia kwa kuzingatia tamko la Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa Tamko Na. 47/237 la 20 Mei, 1993.

Ofisa Ustawi wa Jamii, Furaha Dimitrios alieleza kuwa zipo sababu nyingi za mifarakano lakini kubwa ni msongo wa mawazo unaoweza kusababishwa na tabia za mazoea pamoja na kipato au hali ya kiuchumi.

“Inawezekana mmoja wa wanandoa ana tabia ambayo inamkera mwingine sasa kama hao wawili hawatakaa waongee...watu wamekuwa wakilazimisha wanandoa waongee matatizo yao, katika hali ya kawaida mtu ukishavurugwa umevurugwa, ni ngumu sana kubaki katika hali ya kawaida ili muweze kujadiliana,” alisema.

Alisema mtu huyo anaweza akaamua kujipa muda ili akae sawa ili aweze kujadiliana na mwenzake, endapo atakutana na kero nyingine anaweza akaamua kukaa kimya jambo ambalo ni gumu pia kwani linamfanya alimbikize matukio hatimaye anapata msongo wa mawazo.

“Kwa hii ni moja ya sababu hadi watu wanafikia hatua ya kuachana au hata kama hawajaachana wanalala vyumba tofauti na mkishaanza kulala vyumba tofauti mtashindwa kulea watoto vizuri. Mnaanza kutengeneza mfano mbovu," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live