Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipanya atua Wasafi Media

Kipanya 0016 Kipanya atua Wasafi Media

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Joto la Asubuhi -E Fm, Musa Kipanya ametangazwa na kukaribishwa rasmi kuwa mtangazaji mpya wa Jopo la Watangazaji wa kipindi cha Good Morning ya Wasafi Fm.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Wasafi Media imeandika ujumbe huu katika hali ya kumkaribisha mtangazaji huyo... "MINYAMA Haiwezi Kwenda Bila MATONGE! Karibu Sana Ndani ya Familia Ya #WasafiMedia na Team #GoodMorning @musakipanya ‘MZEE WA MATONGE‘.

Rasmi , Kuanzia Sasa ni NYAMA TONGE Jumatatu Mpaka Ijumaa Kuanzia Saa 11 Alfajiri Mpaka Saa 2:30 Asubuhi Kupitia GOODMORNING ya @WasafiFM."

#KaribuMzeeWaMatonge #HiiNiYetuSote

Unadhani nani anaachilia kitengo katika jopo la watangazaji wa Good Morning ili nafasi yake kukaimiwa na Musa Kipanya?

Tuandikie maoni yako kuhusiana na hili!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live