Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Kim Kardashian amtolea udenda Jude Bellingham

Jude Kim Kim Kardashian amtolea udenda Jude Bellingham

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

habari ndo hiyo. Mrembo, Kim Kardashian ameripotiwa "kumzimia" kiungo wa Real Madrid na England, Jude Bellingham.

Bellingham kwa sasa ni balozi wa kampuni ya mitindo ya Skims. Na mrembo, Kim, 43, amekuwa akiposti picha tofauti za kiungo Bellingham, 20, kwenye mitandao yake ya kijamii wakati akifanya shughuli za uanamitindo na kampuni hiyo.

Kim, ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano na rapa Kanye West alifichua kufurahishwa na kitendo cha Bellingham kuwa balozi wa kampuni ya Skims ambayo inasimamiwa na mrembo huyo matata kabisa.

Lakini, chanzo kimoja kiliiambia Heat Magazine kwamba mrembo Kim si tu anavutiwa na umaarufu wa Bellingham bali kuna kitu kingine kimejificha nyuma, kwamba ana mahaba mazito kwa staa huyo wa Los Blancos.

Na kwamba kinachoelezwa kama Bellingham asingekuwa kwenye uhusiano na mwanamke mwingine, basi Kim angejichomeka fasta.

Chanzo hicho kilifichua: "Kumpata Jude kwenye kampuni ya Skims lilikuwa dili kubwa. Ni moja ya watu wanaofanya vizuri kwenye soka, ni usajili mkubwa kwa Kim. Anaishi Madrid na Kim ameshafahamu yupo kwenye uhusiano, la isingekuwa hivyo, sio siri tena, Kim angejichomeka."

Chanzo kilibainisha kwamba Kim amekuwa hamalizi maneno ya kuhusu mvuto alionao Bellingham.

Bellingham kwa sasa yupo kwenye uhusiano na mrembo wa Kidachi, Laura Celia Valk. Walifanya uhusiano wao kuwa siri hadi hapo ulipokuja kufahamika Aprili, mwaka huu. Na mrembo Kim wala hahofii kuonekana mkubwa kwa kijana mdogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live