Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kardashians nchini India kuhudhuria harusi ya mtoto wa bilionea Ambani

Kim Kardashian Mavazi Kardashians nchini India kuhudhuria harusi ya mtoto wa bilionea Ambani

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kim na Khloe Kardashian wamekuwa miongoni mwa watu mashuhuri duniani walioonekana nchini India siku ya Ijumaa kuhudhuria sherehe ya harusi ya siku tatu iliyoandaliwa na tajiri zaidi barani Asia Mukesh Ambani.

Mtoto mdogo wa Ambani Anant na mchumba wake Radhika Merchant, wote wenye umri wa miaka 29, watafunga ndoa wikendi hii katika mji mkuu wa kifedha Mumbai kufuatia miezi kadhaa ya karamu za kabla ya ndoa ambazo zimeweka alama mpya katika ndoa ghali duniani.

Sherehe za awali zilijumuisha safari ya Uropa kwa wageni 1,200, na familia ya Ambani na maonyesho yaani perfomance ya nyota wa R&B Rihanna na Justin Bieber kutokea Kanada.

Kardashians ndio wa hivi punde katika safu ndefu ya VIP maarufu wa kigeni kuonekana.

Dada mkubwa Kim alishiriki kwenye ya Instastory inayoonyesha gari lake likiwa na wapiga picha wa Kihindi muda mfupi baada ya kuwasili na ndugu zake wote wakipokea vitambaa vya maua kutoka kwa wafanyakazi katika hoteli yao ya kifahari huko India.

Mawaziri wakuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson na Tony Blair pia walionekana na wanahabari wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mumbai kabla ya sherehe kuanza baadaye Ijumaa.

Mnamo Juni, wanandoa walianza safari ya siku nne ya Bahari ya Mediterania, ambapo mwimbaji Katy Perry alitumbuiza huko Cannes.

The Backstreet Boys, rapa wa Marekani Pitbull na tenisi wa Italia Andrea Bocelli pia walitoa burudani.

Kama utakumbuka vizuri wageni waalikwa maarufu katika sherehe za awali ni pamoja na mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg na binti wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Ivanka, pamoja na nyota wengine wengi na matajiri nchini India.

Sherehe zenye za wiki hii zinatazamiwa kuwa kubwa na kuteka hisia za wengi, huku watu mashuhuri zaidi, wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa duniani wakiingia katika jiji kuu la Mumbai .

Watu wakubwa wanaojihusisha na teknolojia duniani, magwiji wa tasnia, mastaa wa Bollywood, wasanii wa pop na wanasiasa pia wanatarajiwa kwa sherehe zinazoandaliwa na bilionea Mukesh Ambani.

Aliyekuwa mgombea urais wa Marekani Hillary Clinton, nyota wa ndondi Mike Tyson na mwigizaji John Cena ni miongoni mwa majina mengine yanayodaiwa kuhudhuria ndoa hii ghali ya dunia.

Ambani, 66, mwenyekiti wa kampuni kubwa ya mafuta kwa mawasiliano ya Reliance Industries, ndiye mtu tajiri zaidi barani Asia kulingana na orodha ya mabilionea ya Forbes, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 114.

si mara ya kwanza kwa tajiri huyu klufanya hivi kwa watot wake kwani Ambani aliwahikufanya harusi ya bei ghali zaidi nchini India kwa binti yake mnamo 2018, ambayo inasemekana iligharimu dola milioni 100 huku mwanamuziki maarufu wa Marekani Beyonce akitumbuiza sherehe hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live