Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jina la album mpya ya ‘KOD’ ya J. Cole alilipata akiwa Tanzania, aeleza ilivyokuwa

Video Archive
Sun, 29 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Rapa kutoka Marekani J. Cole ameweka wazi kuwa wazo la jina la album yake mpya ya ‘KOD’ alilipata akiwa katika visiwa vya Zanzibar mapumzikoni.

Tokeo la picha la J COLE kod

J. Cole amethibitisha hilo jana Aprili 27, 2018 kwenye ukurasa wake wa Twitter akijibu maswali ya masgabiki wake ambapo moja ya mashaabiki hao alimuuliza “Jina la album yako ulilipata baada au kabla ya kumaliza kurekodi?”.

J. Cole alimjibu shabiki huyo kwa kumwambia kuwa “Wakati nikiwa Zanzibar nikirekodi baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album. Nilijiuliza album hii nitaipa jina gani? lakini ghafla nikajikuta naipa jina hilo (KOD). Swali nililojiuliza jina hilo lina maana gani?.Lakini baadae nikapata maana tatu ya jina hilo na kuziweka kwenye mdundo (Yaani wimbo wake wa Windows Pain).



Album mpya ya ‘KOD’ ni album ya tano kwa rapa J Cole na ameiachia Ijumaa iliyopita Aprili 20, 2018. Unaweza ukasikiliza wimbo huo wa Window Pain ambao umeeleza maana ya jina la ‘KOD’ .

Chanzo: bongo5.com