Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jacqueline Mengi awataka vijana kusimamia ndoto zao

50700 Pic+jack

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jacqueline Ntuyabaliwe ambaye ni mke wa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, amewashauri watu kutotaka kufikia mafanikio ya watu ambao wanawaona kwenye mitandao ya kijamii.

Ameyasema hayo leo Ijumaa, Aprili, 5, 2019 alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha XXL kinachorushwa na kituo cha Clouds kuelekea siku ya malkia wa nguvu.

Badala yake Jacqueline amesema kuna watu ambao wana mafanikio ambao wamekuzunguka unapoishi na wanafanya vizuri kuliko hata hao unaowaona kwenye mitandao ya kijamii.

“Tusiangalie wanaoonekana sana, kuna ambao wapo kwenye jamii zetu na hawazungumzi chochote lakini wana mafanikio, hivyo tusihangaike sana kuangalia wale maarufu mitandaoni,” amesema Jacqueline ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2000.

Pia jingine amesema ni muhimu kusimamia kwanza katika ndoto yako kabla hujamtazama mwingine kwani hata yeye alipotaka kufungua kampuni ya kutengeneza samani ya Amorette, hakuwahi kusikia kuna mwanamke anafanya kazi hiyo bali ilikuwa ndoto zake.

“Tangu nikiwa mdogo nilipenda sana kazi za kuchora na ndoto yangu siku moja ilikuwa kuja kuwa na duka la samani, ninashukuru hilo limetimia,” amesema.

Related Content

Hata hivyo Jacqueline amebainisha kuwa kupitia kampuni yake hiyo ya samani ameajiri watu 20 na pia wamekuwa wakitoa mafunzo kwa vijana hususani wa Veta.

Wakati kuhusu bei alisema ni za kawaida kuliko watu wanavyofikiria huku malighafi nyingi zikiwa zinatoka Tanzania kasoro vitambaa ambavyo vinatoka nchi mbalimbali.



Chanzo: mwananchi.co.tz