Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Idadi ya watu wanaochukia Tattoo walizochora yaongezeka

Tattooo Idadi ya watu wanaochukia Tattoo walizochora yaongezeka

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kulingana na uchunguzi wa kitaifa uliyofanywa na ‘Advanced Dermatology’ kutoka Illinois, Marekani umebaini kuwa idadi ya wanaochukia tattoo walizochora yaongezeka.

Katika uchunguzi huo uliyofanywa kwa kipindi cha mwaka mmoja ulibaini kuwa idadi ya waliotaka kufuta tattoo zao imefikia asilimia 51 ikiipiku idadi ya awali ikiwa asilimia 15.

Aidha Dk. Alissa Lamoureaux, daktari wa ngozi aliyeidhinishwa na bodi huko #Shrewsbury, alieleza kuwa watu hutaka kuondolewa tattoo zao kutokana na umri wao kwenda.

“Ni watu wa umri kuanzai 30-40, huwenda walichora #tattoo hizo wakiwa wadogo na sasa wanaona ni kama fashioni hiyo imepitwa na wakati katika umri wao” amesema.

Vipi bado unamapenzi na tattoo yako, au nawewe unataka kuifuta?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live