Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Horombo; Mwanadamu aliyeua tembo kwa mikono

Tembo Temboooo Tembo

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 1800 alitokea chifu aliyejulikana kama Mangi Horombo kutoka Mashariki mwa mlima Kilimanjaro. Horombo alikuwa mwanadamu mrefu sana katika historia ya Wachaga, akiwa na urefu wa futi 8. Yaani akiingia Kaburini anatokea juu futi mbili zaidi.

Alikuwa hodari na mwamba wa vita. Alipokuwa kijana mdogo, Nchi ya Rombo ilikuwa chini ya Utawala wa Mamba (Mangi wa Marangu), isipokuwa eneo la Usseri (nyumbani kwetu). Usseri kwa sasa ni Tarafa ilikuwa nchi iliyojitegemea.

Eneo lingine lilokuwa na nguvu ni Nchi ya Chimbili mbele kidogo ya Mkuu, hapa aliishi Mzee Moosinyi. Moosinyi alipigana vita muda mrefu na Mamba lakini akashindwa.

Vita yao ilitokana na mzozo wa mifugo. Wamarangu walipeleka mifugo yao Rombo ili warombo waifuge, ikifika Disemba wanaenda kuchukua mifugo. Warombo walikerwa na tabia hiyo ya mabavu ya kuwalisha mifugo wa wamarangu bila malipo au faida.

Horombo alikuwa mjukuu wa Mzee Moosinyi akaamua kuendeleza uhasama wa Babu yake dhidi ya Mangi Mamba

Horombo akawawapiga wamarangu waliofuata mifugo, na kutuma taarifa marangu kuwa kuanzia wakati huo mifugo iliyopo Rombo sio mali zao na ni marufuku kupeleka mifumo Rombo. Horomba akatangaza kuwa nchi ya Keni ni Nchi inayojitegemea sio koloni la Mamba tena.

Horombo akashinda vita hivyo. Unaambiwa Mangi Horombo alikuwa na uwezo wa kuua Simba au mnyama yoyote wa porini. HOROMBO ANA HISTORIA YA KUUA TEMBO YEYE MWENYEWE.

Horombo ndiye Mangi wa kwanza kuanzisha wazo la kujenga himaya ya Wachaga. Alianza ujenzi wa uzio wa kuzunguka Keni lakini kabla ya kufanikiwa kufanya hivyo alivamiwa na wamasai.

Kwenye vita hivyo Horombo alishinda, lakini wakati anarudi nyumbani kutoka vitani, Mmasai mmoja aliyekuwa chini hajafa akamchoma mkuki wenye sumu.

Horombo alipogundua amechomwa mkuki wenye sumu na hawezi kupona kwa haraka akawaagiza vijana wake wamuue kisha kichwa chake kichomekwe kwenye mkuki, ili wamasai wakijitokeza wanyanyue kichwa chake nyuma ya Ukuta waliojenga. Kwa kuwa wamasai walimuogopa Horombo walipokuwa wanaona sura yake walikimbia.

Baada ya kifo chake utawala wake ulikufa, wakaibuka mangi wakubwa kama Sina na Rindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live