Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hizi ndizo nchi zinazoongoza kwa ulevi wa pombe duniani

Pombe Kifo Ulevi wa pombe

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani, WHO linasema kuwa watu milioni 2.6 hufariki dunia kutokana na unywaji pombe kila mwaka.

WHO inasema unywaji pombe huongeza hatari ya kupata magonjwa hatari kama vile magonjwa ya moyo, saratani ya ini na afya mbaya ya akili.

Haya yamo katika ripoti mpya iliyotolewa na tume ya unywaji pombe na afya na huduma kwa waathirika wa dawa za kulevya.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa watu milioni 400 wanaishi na pombe na dawa nyingine za kisaikolojia.

“Kati ya idadi hii, watu milioni 209 wanategemea kunywa pombe ili kuishi,” ilisema ripoti hiyo.

Mkuu huyo wa Shirika la Afya Duniani amesema kuwa unywaji wa pombe ni hatari sana kwa afya za watu na husababisha madhara mengi kwa watu wanaokunywa pombe zaidi.

"Lazima tusimame kuondoa unywaji pombe, ikiwa tunataka kuboresha afya na ustawi wa watu wetu," alisema rais wa WHO.

Ripoti hiyo pia inaonesha kuwa nchi za bara la Ulaya ndizo zinazoongoza kwa unywaji wa vileo, ambapo inakadiriwa kuwa wastani wa pombe anayokunywa mnywaji kila mwaka ni lita 9.2.

Kisha kuna bara la Amerika ambapo kila mlevi hunywa lita 7.5 kwa mwaka. 1. Romania Romania, ambayo iko sehemu ya kusini-mashariki mwa Ulaya, ina idadi kubwa zaidi ya vileo kulingana na takwimu za WHO.

Romania, yenye idadi ya watu milioni 19.12, ni maarufu kwa baa za mvinyo.

2. Georgia Georgia, ambayo ni sehemu ya Muungano wa zamani wa Soviet uliovunjika, ipo kati ya Ulaya na Asia.

Ni nchi yenye wakazi wapatao milioni 3.8 yenye historia tajiri ya kitamaduni na ambayo ni maarufu kwa kuzalisha pombe duniani.

Guinness Book of World Records hapo awali iliorodhesha nchi hiyo kama nchi inayodhibitiwa zaidi ulimwenguni.

3. Jamhuri ya Czech Takwimu za WHO zimeitangaza Jamhuri ya Czech kuwa nchi ya tatu kwa walevi wengi duniani.

Pia ni nchi ya kwanza kutumia pesa nyingi zaidi kununua pombe duniani, ambapo mwaka 2019 ripoti ya takwimu za Ulaya inaonesha kuwa nchi hiyo ilitumia takribani dola bilioni nne kununua pombe.

Ripoti ya WHO pia inaonesha kuwa wengi wa watu wanaokufa kutokana na kunywa pombe hufa kwa kunywa pombe iliyochafuliwa.

Jinsi pombe iliyochafuliwa inavyoua watu Katika baadhi ya nchi, pombe huuzwa kwa wanywaji mitaani. "Watu wengi wanaokunywa pombe iliyochafuliwa hufa, kwa hivyo nilifikiria pia kuwa sitaishi," alisema Satya, mwanamke ambaye anaendelea kupata nafuu hospitalini, kutokana na ugonjwa aliopata baada ya kunywa pombe iliyochafuliwa, nchini India.

Satya alikuwa miongoni mwa watu 219 waliolazwa hospitalini wiki iliyopita katika jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu baada ya kunywa pombe iliyochafuliwa.

Satya anasema kuwa ana bahati ya kuwa hai baada ya kunywa pombe iliyochafuliwa ambayo ilisababisha vifo vya watu wengi TAMIL Takribani watu 57 walipoteza maisha baada ya kunywa pombe hiyo iliyochafuliwa.

"Nimekuwa nikinywa pombe kwa karibu miaka 20. Kila siku ninayokaa hospitalini ninahisi kama mwaka. Nimeacha kunywa pombe,"

Watu ambao maisha yao yaliokolewa baada ya kunywa pombe iliyochafuliwa wanaendelea kusalia katika hospitali ya Tamil Nadu TAMIL Nchi ambazo uchafuzi wa pombe huua zaidi Takribani watu 900 hufa nchini Urusi kila mwaka kutokana na kunywa pombe iliyochafuliwa, kulingana na shirika la haki za watumiaji.

Huko Iran, watu 44 waliripotiwa kufa mnamo 2020, kwa sababu ya kunywa pombe iliyochafuliwa.

Huko Indonesia, takribani watu 45 walikufa mnamo 2018.

Uchafuzi wa pombe hupatikana kwa wingi katika bia inayotengenezwa nyumbani, kutokana na hatua duni za usalama zinazochukuliwa wakati wa kuichanganya.

Utafiti umeonesha kuwa pombe iliyochanganywa katika kampuni ya kuchanganya pombe ina ubora wa juu kuliko ile iliyochanganywa nyumbani.

Kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa, walevi hao wameingia kwenye matumizi ya bia iliyochanganywa nyumbani, kwa sababu hawana uwezo wa kununua ile iliyochanganywa na kampuni.

Watu 170 walikufa mnamo 2011 katika jimbo la Bengal mashariki mwa India, huku zaidi ya 100 walikufa katika jimbo la Gujarat mnamo 2009.

Pia huko Mumbai watu 100 walikufa mnamo 2015.

Mnamo 2022, wachunguzi walipata miili ya watu 21 waliokufa katika kilabu cha usiku nchini Afrika Kusini. Mazishi ya pamoja yalifanyika kwa vijana waliofariki nchini Afrika Kusini mwaka 2022.

Nchi za Kiislamu zinapiga marufuku unywaji pombe Nchi za Kiislamu zinakataza kunywa pombe, kwa sababu katika Uislamu kunywa pombe ni haramu.

Wataalamu wanasema katika nchi za Kiislamu kama vile Iran na Indonesia kuna sheria na kanuni kali za baa. Hatua kali husaidia kupunguza idadi ya baa za pombe nchini.

Ama watu wanaokunywa pombe huwa wanakwepa kuomba msaada wanapokunywa pombe na kuogopa kugongana, kwa sababu ya adhabu itakayowapata, iwapo watabainika wamekunywa pombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live