Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hii ndio Talaka mbaya kuwahi kutolewa (+Video)

Talakaaaaa Hii ndio Talaka mbaya kuwahi kutolewa

Thu, 23 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 1994, Mwanaume aliyeitwa Gabriel alikutana na mrembo Christina Carta katika party moja huko jijini New York, Marekani.

Walipendana na wakaamua kuoana huku wakila bata na kukwea na ndege huku na kule, ingawa Gabriel alimzidi umri christina kwa miaka 30. Hata hivyo waliishi kwenye ndoa yenye furaha na upendo wa kila aina.

Miaka 20 baadae, Christina aliletewa documents za malipo ya kodi ya nyumba yao waliyopangisha huko Manhattan. Cha kushangaza jina lake halikwepo kwenye zile documents. Kwa mshangao mkubwa, christina alimwajiri mwanasheria ili achunguze lile jambo.

Baada ya uchunguzi, mwanasheria alikuja na jibu kuwa, Mwenzi wake Gabriel alishampa talaka miaka 20 iliyopita bila yeye kujua. Ilikuwa hivi, Miezi minne baada ya ndoa yao, Gabriel na Christina walienda nchi ya Dominican Republic kula maisha.

Nchi ya Dominican ndio nchi pekee duniani inayomruhusu mtu kutoa talaka bila kumpa taarifa mwenzi wake. Gabriel alijua fika kuwa Christina hamkupenda kwa dhati ila alikubali kuolewa nae ili apate mali, hivyo alimpa talaka mapema ili baadae asimje kudai mali wakati atakapoomba talaka.

Kwahiyo, waliporudi Marekani, Gabriel aliendelea kuishi na Christina kwa miaka 20 kama mtalaka wake bila Christina kujua.

Cristina Carta akiwa na umri wa Miaka 59, alimshtaki mume wake mwenye umri wa miaka 90, Gabriel Villa, na kudai fidia kubatilisha talaka ambayo hakuwahi kuijua - na kumzuia kuuza nyumba waliyoishi Lakini mahalama ilikataa na kusema alishapewa Talaka mika 20 iliyopita.

View this post on Instagram

A post shared by Manara TV (@manaratv__)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live